KESHO kikosi cha Yanga kitakuwa na mechi ya Ligi Kuu Bara itakayochezwa Uwanja wa Majaliwa dhidi ya Namungo FC.
Namungo FC ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 49 kibindoni inakutana na Yanga iliyo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 50 kibindoni.
50 za Yanga zimepatikana baada ya timu hiyo kucheza mechi 26 huku 49 za Namungo zikipatikana baada ya mechi 27.
Vita kubwa inatarajiwa kuwa leo kutokana na ushindani wa nafasi tano za juu huku kila kocha akiwa na mipango yake ya kusepa na pointi tatu.
Hitimana Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo ambaye atakuwa mwenyeji amesema kuwa anaamini mchezo utakuwa mzuri na wenye ushindani kikubwa ni kusubiri kuona vijana wake watafanya nini ndani ya dk 90.
Luc Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa anawaamini wachezaji wake hawatamuangusha kutokana na kutokana na kutoka kupoteza mbele ya KMC kwa kufungwa bao 1-0.
Eymael anajivunia uwepo wa nyota wake David Molinga ambaye ni kinara wa kutupia akiwa nayo nane na pacha wake Patrick Sibomana mwenye mabao matano na pasi moja ya bao.
Nawtakia kila LA hero yanga.
ReplyDeleteNamungo tunakutakia kila la kheri na muteremshe mvuwa ya magoli kama yale Kagera Sugar tulale usingizi mtamu kwasababu mnao uwezo wa kutufulaisha
ReplyDelete