March 14, 2020

PATRICK Aussems, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba ambaye alipigwa chini akiwa ameiongoza timu hiyo msimu huu wa 2019/20 kwenye mechi 10 amesema kuwa itakuwa ngumu kwa Klabu ya Simba kuvunja rekodi ya kutinga hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Aussems, raia wa Ubelgiji alipokuwa na Simba aliifikisha kwenye hatua hiyo ya robo fainali jambo analoamini kuwa itakuwa ngumu kwa timu hiyo kufika kwa wakati huu.

" Malengo yao najua  ni kuona wanafanikiwa kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao na hilo lipo mikononi mwao kwani wanaongoza ligi wakiwaacha wapinzani wao lakini kufikia hatua ya robo fainali itakuwa ngumu.

"Ninajua  haliwezi kutokea kwa sababu siasa za viongozi na kila mmoja atahitaji kuona cha kwake ndiyo sahihi na ugumu wa michuano kimataifa kwa timu zenye malengo upo wazi ila siyo Simba," amesema.


Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 71 kibindoni imecheza mechi 28 huku Azam FC inafuata nafasi ya pili na pointi 54 zote zimecheza mechi 28.

4 COMMENTS:

  1. Huyu kocha amekuwa mropokaji kama kweli kasema hivyo. Anajua wachezaji Simba itaowasajili kuziba mapungufu?Anajua nä kutathimini vipi matayarisho ya Simba kwenye michuano hiyo?

    ReplyDelete
  2. Anatapatapa alikuwepo Simba akazembea na jeuri juu. Labda anafikiri ni yeye tu anaeweza kuipa Simba mafanikio kwa hivyo aitwe tena.Binafsi namuona kocha mpya wa Simba na benchi lake la ufundi wapo imara zaidi kuliko yeye.

    ReplyDelete
  3. ilipofika fainali alikuwepo si ni hii hii simba na watu ni wale wale

    ReplyDelete
  4. Kichwa cha habari sio sahihi..... Aliyekuwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic