March 24, 2020

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Ditram Nchimbi amesema kuwa miongoni mwa sababu zilizoifanya timu yake kusepa na pointi tatu mbele ya Simba Machi 8 Uwanja wa Taifa ni kukamia kwa mabeki wa Simba mchezo huo mwanzo mwisho.

Nchimbi alikuwa msumbufu kwenye mchezo huo ambapo licha ya kushindwa kufunga aliwachosha mabeki wa Simba waliokuwa wakimkaba kwa zamu ambapo aliwekwa kwenye uangalizi mkubwa na Pascal Wawa.

Nchimbi amesema: "Mabeki wa Simba walipania mchezo tangu tunaanza walikuwa wanaamini kwamba tutawaogopa jambo ambalo halikutokea na mwisho wa siku wakapoteza nasi tukashinda.

"Pascal Wawa alikuwa anaamini kwamba nitaingia uwanjani nikiwa na hasira kwa kuwa alinichezea rafu kwenye mchezo wetu uliopita kumbe mimi nilikuwa nimesahau na nilingia nikiwa na kazi moja ya kuipa timu matokeo.

"Hasira za mabeki wao ziliwaponza ila kidogo Erasto Nyoni alikuwa anatumia akili tofauti na Wawa ambaye alikuwa anatumia nguvu hilo lilitupa nguvu," amesema.

Mchezo wa kwanza Yanga ikiwa ugenini ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 Januari 4 Uwanja wa Taifa na mchezo wa pili Yanga ilisepa na pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0.

2 COMMENTS:

  1. Acheni unazi ivi kati ya simba na yanga aliyekua amekamia mechi ni nani?wenzenu simba wamecheza mpira wa kiwango chao na ndiomana ukiacha mechi ya simba na yanga bado waliendelea kushinda mechi yao iliyofuata tena kwa magoli mengi mpaka aibu,je kilichowakuta nyinyi baada ya mechi ya watani mnakijua?na je mnajua sababu kwanini mlifungwa na tena kwakucheza chini ya kiwango?unajua kwanini mechi iliyofuata mlisuluhu?hapo ndipo utakapopata majibu yatakayopingana na hoja yako kwamba eti simba walikamia mechi,ule ni mpira wa simba yani ni kawaida ya simba kucheza kiwango kile,na walichokifanya simba nikusoma akili za yanga basi na walivyogundua wamekamiwa ndipo walipoamua kurelax kama unabisha chunguza haswa kipindi cha pili,madhara yakukamia mechi ni makubwa sana na mara nyingi yanakua ni hasara inayoigharimu timu maana wachezaji walijitoa mhanga kwakutumia nguvu za ziada hatimae mnakuja kufungwa mechi kibao kama kilichowakuta yanga,kwa mpira mliocheza na simba kama mngelikua mnacheza vile kila siku leo hii mngekua ndio mpo pale kileleni mkisubiri kutawazwa kuwa mabingwa wa VPL,lakin mnakamia mechi ya watani alafu madhara yake ndio haya,poleni sana maana mtaendelea kufungwa sana tena mpaka mtachukiana wenyewe,POVU RUKSAAAAAAAAAAA.

    ReplyDelete
  2. HA HA HA HA HA HA HA NACHEKA KWA DHARAU,LIFE IS SIMPLE,MWANDISHI ULIKUA WAPI SIKU ZOTE HIZO LEO NDIO UNALETA MADA ZA SIMBA NA YANGA?HII NAYO NI SHOTI INA MAANA WEWE UNAIHUJUMU YANGA MAANA KINACHONADIWA KUHUSU YANGA NI KINYUME NA UHALISIA SASA HUONI KWAMBA UNATENGENEZA BOMU AMBALO LITAKUDHURU MWENYEWE BAADAE,YANGA TUNAYOIFAHAMU SIO YANGA INAYONADIWA KUA BORA KIASI HICHO NA NDIOMANA HATA MATOKEO YAKE YAMEKUA YAKUSUASUA,ILA NI WAKATI TU HAUJAFIKA WA WATANZANIA KUJIELEWA NAKUJITAMBUA KUHUSU SOKA,YANGA WAMEKUA WAONGO SANA TENA WABABAISHAJI NA WATU WENYE KUTUMIA MBINU NYINGI SANA KUJIKUSANYIA MASHABIKI NA MTAKUJA KUGUNDUA VYOMBO VINGI VYA HABARI VIMELIPWA ILI KUFICHA UKWELI KUHUSU YANGA NAKUINADI YANGA KINYUME NA UHALISIA,TUMUOMBE MUNGU ILA IPO SIKU UKWELI UTAFAHAMIKA NA WENGI MTARUDI NYUMBANI MAANA MADUDU YANAYOENDELEA HAPO NAAMIN KABISA HAKUNA MSHABIKI NA MPENZI WA MPIRA ATAWEZA KUENDELEA KUWEPO PALE TU ATAKAPO GUNDUA NAKUJUA KINACHOENDELEA YANGA.MUNGU IBARIKI YANGA YA VIJORA MUNGU IBARIKI SIMBA YA UBINGWA,NA SAFARI HII SIJUI MTAKATA CHA RANGI GANI MAANA MNAPENDA KWELI KWENDA USIKU WA ZAWADI NA VIJORA VYENU VYA SISIEMU.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic