March 15, 2020

ERICK Kabamba, Yikpe Gnamien,David Molinga, ni miongoni mwa wachezaji wa kigeni ambao wanajadiliwa na uongozi wa Yanga ili kujua hatma yao ndani ya kikosi hicho ambacho kinaelekea kufanya mabadiliko makubwa.

Habari zinaeleza kuwa licha ya Molinga kuwa mfungaji namba moja wa kikosi hicho bado, Kocha Mkuu Luc Eymael hajaelewa mchango wake akiwa uwanjani jambo linalompasua kichwa.

"Kuna wachezaji ambao wataondoka baada ya msimu wa Ligi Kuu Bara kuisha kinachosubiriwa ni ripoti kutoka kwa kocha atakachokisema ndicho kitafanyika lakini kwanza tuwatazame kwa muda huu," kilieleza chanzo hicho.

Yanga ikiwa imecheza mechi 26 imefunga mabao 30 na kinara wa kutupia ni Molinga mwenye mabao 8 akifuatiwa na Patric Sibomana mwenye mabao matano.

2 COMMENTS:

  1. Nyinyi munautaka ubingwa na wachezaji Hao pamoja na Molinga ndie mnaemtegemea na mwenye mabao mengi mnawataja waziwazi kuwatimua, wachezaji watakuwa na moyo gani ndani ya timu. Kweli hiyo akili

    ReplyDelete
  2. UNAWALAUMU VIONGOZI WA YANGA WAKATI HIZI NI HABARI ZA MAGAZETI NA SIO RASMI KUTOKA CLUM YA YANGA !!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic