NYOTA wa
kigeni ndani ya kikosi cha Simba wameonekana na balaa kwenye kucheka na nyavu
huku wakiyapoteza jumla mabao yaliyofungwa na wapinzani wao Yanga.
Simba ikiwa
ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 28 imefunga mabao 63
ambapo wazawa wamefunga mabao 22 na wageni wamefunga mabao 41 wakiipoteza ile safu ya Yanga ambayo kwenye mechi 26 imefunga mabao 30.
Kinara wa
kutupia mabao kwa wageni ambaye pia anakimbiza kwenye ligi ni Meddie Kagere
raia wa Rwanda mwenye mabao 19 akifuatiwa na Deo Kanda raia wa Congo mwenye
mabao 7, Francis Kahata raia wa Kenya ametupia mabao manne huku Luis Migussone
raia wa Msumbuji, Gerson Fraga raia wa Brazil
wakitupia mabao matatumatatu kila mmoja.
Sharaf Shiboub raia wa Sudan na Clatous Chama
raia wa Zambia wakitupia mabao mawilimawili, Tairone Santos raia wa Brazil ametupia bao moja.
Kwa upande wa wazawa Miraj Athuman ‘Sheva’ na Hassan Dilunga wanaongoza jahazi kwa kutupia mabao sita kila mmoja wakifuatiwa na nahodha John Bocco mwenye mabao manne, Jonas Mkude na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ wametupia mabao mawilimawili huku Ibrahim Ajibu na Erasto Nyoni wakitupia bao mojamoja.
0 COMMENTS:
Post a Comment