DUNIA kwa
sasa inasumbuka na janga la kusambaa kwa Virusi vya Corona ambavyo mpaka sasa
inaelezwa Italia imechukua vifo vya watu wengi zaidi ya nchi nyingine.
Virusi hivyo
ambayo husababisha ugonjwa wa Covid-19, vimefanya shughuli mbalimbali kusimama
duniani ikiwemo michezo.
Italia,
Ufaransa, Ujerumani, Hispania, Uturuki na nchi zingine barani Ulaya
zimesimamisha ligi zao.
Afrika pia
mambo yapo hivyohivyo, kuanzia Shirikisho la Soka Afrika (Caf) hadi
mashirikisho mengine ya soka kwa nchi mbalimbali yamesimamisha ligi zao.
Afrika
Kusini, Morocco, Botswana, Zambia, Kenya, Uganda na hapa nyumbani Tanzania ni
baadhi tu ya nchi zilizosimamisha ligi zao lakini kwa jumla ligi za soka
zimesimamishwa kwa sasa.
Sababu kubwa
ni katika kupambana na janga hili ambalo kwa Tanzania tulitangaziwa lilikuwa
limeingia takribani wiki sasa.
Muda mchache
baada ya virusi hivyo kuripotiwa kuingia Tanzania, Serikali ikatoa tamko la
kuagiza kusitisha mikusanyiko isiyo ya lazima.
Katika hilo,
ndipo ikatoka kauli ya kusimamisha michezo kwa siku 30 kuanzia Machi 17, mwaka
huu. Miongoni mwa michezo iliyosimamishwa, soka ni mojawapo.
Pia Serikali
ikafunga shule na kutoa tahadhari kwa wananchi wake kujikinga na virusi hivyo,
pia zikielezwa njia za kukabiliana na kusambaa kwake.
Safari
zisizo za lazima za nje ya nchi zimezuiwa. Wananchi wametahadharishwa
wasisafiri nje ya nchi kama safari zenyewe hazina ulazima sana, lakini kama
utasafiri, fuata maelekezo kutoka kwa wataalamu wa afya ili iwe rahisi kwako
kujiepusha kuambukizwa Corona.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) nalo
likakazia hapohapo, kusimamishwa kwa ligi zake kukaambatana na kutoa tahadhari
kwa wachezaji wa kigeni wasirudi nchini kwao ili tu kuwalinda wao na jamii zao.
Kauli ya
Rais wa TFF, Wallace Karia aliyosema itawazuia wachezaji wa kigeni waliokwenda
kwao kipindi hiki, inafikirisha sana.
Tangu kauli
hiyo itoke, kumekuwa na mvutano, wapo wanaoungana naye, pia wapo wanaompinga.
Yote kwa
yote tunapaswa kuelewa kwamba kauli yake ilikuwa ni sehemu ya kutoa tahadhari
juu ya janga tulilokuwa nalo.
Hivi itakuwaje
ikitokea mchezaji, kiongozi na kocha wa timu fulani hapa Bongo akirudi akiwa na
maambukizi hayo halafu akajichanganya na wenzake kabla ya kugundulika. Itakuwa
balaa.
Tunaambiwa
virusi hivyo vinasambaa kwa njia mbalimbali ikiwemo hewa, sasa huyo mtu akiwa
kambini na kujumuika na wenzake kwa muda mrefu, akija kugundulika atakuwa
amewaambukiza wenzake wangapi?
Watanzania
tuache ushabiki, kwenye mambo siriazi tuwe siriazi kweli, tuache utani.
Kwanini asiseme kwamba wachezaji wataorudi wapimwe kabla ya kujumiika na wenzao ?Utazuia watu kwenda kwao?Wachezaji wataokwenda Mwanza, Iringa na wengineo wanaotoka timu mbali mbali nani ana uhakika watakuwa salama?Ingekuwa busara TFF iseme timu zipime wachezaji wao wote kabla ya kuanza mazoezi. Wachezaji wengine duniani wamekwenda kwao kwenye kipindi hiki kigumu.
ReplyDeleteBaada ya kusimamisha ligi, tamko la wachezaji wasiende makwao halikuwepo bali limetoka baada ya wachezaji wamekwisha enda makwao, mfano tuweke ushabiki pembeni, tangia nianze kuangalia wachezaji na mienendo yao sijawahi kumuona kagere akishtumiwa hivyo najua kama tamko lingetoka mapema sidhani kama kagere angetoka maana ni mtu ambae amekuwa na mienendo ya nidhamu tangia akiwa anacheza ligi nchini kwao mpaka sasa yukko hapa. Hvyo karia atumie busara tamko limetoka tayari wengne wamekwisha ondoka sasa nani alaumiwe?
ReplyDeleteChakufanya nikuwataka wachezaji kuchukuliwa vipimo na kusubiri kwa mda wa siku 14 kabla ya kujiunga na wenzao, na huo ndio utaratibu.
Delete