MZAMIRU Yassin, kiungo wa Simba anatarajia kuanza kuonyesha makeke yake leo Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara iwapo Kocha Mkuu Sven Vandnbroeck ataamua kumtumia.
Yassin ilielezwa kuwa aliumia mara baada ya sare ya kufungana mabao 2-2 mbele ya Yanga mchezo uliochezwa
Januari 4,2020 Uwanja wa Taifa.
Leo Simba itakuwa kazini ikimenyana na KMC mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa majira ya saa 2:00 usiku.
Yassin amesema: 'Kwa sasa nipo fiti na ninaendelea vizuri, daktari ameniambia ninaweza kuanza kucheza hivyo mwalimu akiamua nitacheza,".
Kabla ya kupotea uwanjani, Yassin alikuwa ametoa pasi tatu za mabao alimpa moja Miraj Athuman kwenye ushindi wa bao 1-0 mbele ya Singida United na mbili alimpa Meddie Kagere kwenye ushindi wa mabao 3-1 mbele ya JKT Tanzania.
0 COMMENTS:
Post a Comment