March 8, 2020



LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa hana mashaka makubwa ya kukutana na timu yoyote Bongo ikiwa ni pamoja na Simba kutokana na kuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kumpa matokeo.

Yanga leo itamenyana na Simba Uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wa pili wa mzunguko wa pili kwa msimu wa 2019/20 ule wa kwanza uliopigwa Januari 4,2020 Simba ilikubali sare ya kufungana mabao 2-2.

Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa anawaamini nyota wake wengi ikiwa ni pamoja na Nchimbi (Ditram), Bernard Morrisons,Haruna Niyonzima na Molinga (David) na Patrick Sibomana.

Nyota hao anaowakubali Eymael wamehusika kwenye mabao 23 kati ya 29 yaliyofungwa na Yanga kwenye ligi msimu huu ambapo Nchimbi amehusika kwenye mabao manne akifunga mawili na kutoa pasi mbili, Niyonzima amefunga bao moja, Morrison kwenye mabao manne amefunga mawili na kutoa pasi mbili za mabao, Molinga ametupia mabao 8, Sibomana ana mabao matano na pasi moja ya bao.

“Mchezo hautakuwa rahisi hilo lipo wazi wao wanajiandaa kushinda nasi pia tunajiandaa kushinda, ila nina wachezaji ambao wana uwezo mkubwa wa kufunga na kutengeneza nafasi nawaamini wengi ikiwa ni pamoja na Nchimbi,Sibomana, Niyonzima,Molinga na Morisson ambaye anapenda kucheza pia na jukwaa,” amesema.

7 COMMENTS:

  1. Pigeni kelele tu ila muda utaongea,na hilo gazeti lenu sijui kesho mtaandika nini maana kusema kweli msimu huu mmeropoka mpaka inatia kichefuchefu,mungu atawalipa sawasawa na kazi ya miguu yenu.tuendelee kuiombea simba kimyakimya kama tulivyokubaliana,msemaji wetu alishasema nakutoa kauli mbiu tuwe wapole wala tusiwajibu kwa maneno maana hiyo ni sifa yakudhihirika ujinga ulionao.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwahyo hapo umekaa kimya au umeropoka!!? Jitahid kuwa na ufahamu kwenye kauli,hapo umeropoka na sio kukaa kimya,mjinga ni yule asiejua kwamba yeye mjinga

      Delete
  2. Majembe haya matatu ya Tampa kiburi Mzungu. MIMI NAHISI MIPINI ITAVUNJIKA

    ReplyDelete
  3. Hii Ni derby tusichukulie poa, suala sio kupngea Sana au kukaa kimya suala Ni Nidhamu ktk mchezo wenyewe.
    Dakika 90 ndio itatoa majibu...

    ReplyDelete
  4. Derby ya saiz simba wamejishusha sana pia haijawa na mbwembwe nying kama iliyopita. Naombea mpira mzuri kwenye maamuzi mazuri yasiyopendelea upande wowote

    ReplyDelete
  5. HAJI MANARA AMESHAJIFUNDISHA ILE MECHI YA MWANZO NA KUJUA KUA KWELI MPIRA UNADUNDA NA CHOCHOTE KINAWEZA KUTOKEA KATIKA MPIRA NDIO MAANA AKASEMA SIMBA KAENI KIMYA AKIWA NA MAANA KUA PIGENI KELELE KAMA KAWAIDA YENU PALE MTAKAPOSHINDA NA SIO SASA MAANA MKIANZA KUPIGA KELELE SASA HALAFU MKAFUNGWA ITAKUA NI SHIDA YAANI ADHABU JUU YA ADHABU NA HATA HIVYO BADO MASHABIKI WA SIMBA WASIOJITAMBUA WANAPIGA KELELE NA TAMBO NYINGI MITAANI .

    ReplyDelete
  6. UKIANZA NA MEDIA ZINAONYESHA AU KUDHIHIRISHA WAZI YANGA NDIO INAONGOZA ZAIDI KWA MANENO NA MBWEMBWE NYINGI LABDA TU UJITOE UFAHAMU KUJITETEA ILA UKWELI UNAUJUA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic