SAFU ya ulinzi ya Yanga iliyo chini Lamine Moro, Kelvin
Yondan na Juma Abdul imekubaliana kuendeleza rekodi iliyojiwekea kwa kucheza
mechi nne sawa na dakika 360 bila kuruhusu bao.
Rekodi hiyo wanaitaka pia kwenye
mchezo wao wa leo dhidi ya Simba inayoongozwa na safu ya ushambuliaji ya Meddie Kagere na kiungo msumbufu Luis Miquissone.
Rekodi hiyo ilianza kuwekwa kuanzia Februari
23 mbele ya Coastal Union 0-0, Februari 26,Gwambina FC 0-1 Februari 29 Alliance
0-2 na Machi 3, Yanga 2-0 Mbao FC, safu yao ya ushambuliaji ilifunga mabao matano
huku makipa wao wakitoka na clean sheet.
Akizungumza na Saleh Jembe, nahodha msaidizi wa Yanga,
Juma Abdul amesema kuwa hesabu zao ni kuona hawaruhusu kupitwa na mpinzani wao hivyo
wamekubaliana kucheza kwa nidhamu.
“Tunatambua ushindani ni mkubwa na kwa namna ambavyo
wapinzani wetu wamepania basi sisi tumekubaliana kuendelea kucheza kwa utulivu na
nidhamu, ukali wa safu yao ya ulinzi haitupi presha kwani mpira ni dakika 90,
mashabiki watupe sapoti,” amesema Abdul.
John Boko ndie atakaeamua mechi hii kama atamka vizuri na wala sio kagere au L Miquissonne.Boko anatakiwa kujitambua na kulazimisha mashambulizi mbele ya mabeki wa Yanga, watachemka tu hasa kama Yondani atacheza. Yanga wanapata kiburi kwa kudhani beki ya Simba ni nyanya ila kama Simba watafanya marekebisho kidogo tu kwenye beki yao basi sioni Yanga akichomoka Taifa. Beki ya Simba inashindwa kujipanga vyema wanapokabiliwa na mashambulizi.Pengine ni tatizo la kipa kushindwa kupanga beki yake. Mara nyingi mabeki wa Simba wamekuwa hawana adabu ya ulinzi na kuacha mianya mingi kwa adui kuataki. Mara nyingi huenda kukaba wote kwa pamoja na wakipitwa hupitwa wote. Na mbaya zaidi mara nyingi wanaruhusu wapinzani wao kuingia kwenye kumi nane wakiwa huru na kuwapa nafasi ya kujaribu kupiga mashuti bila kubughudhiwa. Taiazo hili ni la muda mrefu kwa Simba labda kwakuwa beki ndio ile ile lakini la kushangaza kwanini wanashindwa kubadilika?
ReplyDeleteUlichokisema mdau hapo juu ni ukweli mtupu nyoni na wawa wanacheza mstari mmoja hawachezi ile tight making.Ndo maana huwa wanapata shida wanapokutana na striker wanaokimbia.Wawa ni mzuri kukaba hivyo angekaa mbele ya nyoni na wahakikishe hawawapi wapinzani kuliona goli.Wakijipanga vizuri kwa uzuri wa Manula wapinzani hawawezi kupata kitu
ReplyDeletesimba anakufunga ukimuogopa lakini ukimkabili ananywea kama simba wa porini hivyo hivyo ukimshikia fimbo tu na kumkabili ananywea na hata kukukimbia !!!!
ReplyDeletePamoja na madhaifu machache kwenye safu ya ulinzi ya Simba;kitakachoweza kuwa changanya Yanga ni mashambulizi ya mfulilizo. Hapo ndo nguvu ya Simba wakiweza ilo Yanga wanalala na viatu mapema.
ReplyDeleteKuitangulia Yanga kwa pointi za kutosha kutaipa Simba ujasiri wa mchezo.
Vinginevyo mchezo utakuwa mgumu.
Kened Juma aaminiwe kwa sasa akimsubiri aliye Coastal Union kwa mkopo ili watengeneze ukuta wa Vijana
ReplyDelete