KUFUATIA
mlipuko wa ugonjwa wa Corona unaoendelea kutokea kwa sasa duniani, makocha wa
timu za Bongo zinazoshiriki Ligi Kuu Bara wameomba ugonjwa huo usitue nchini na
kuwaombea wagonjwa wapone mapema ili kurejea kwenye ubora wao.
Virusi hivyo
ambavyo vilianza kuenea kwa kasi mwezi Januari vimekuwa ni hatari duniani
ambapo kwenye sekta ya michezo kumesababisha ligi kubwa kusimamishwa ikiwa ni
pamoja na Serie A, huku ile ya England nayo ikisimaishwa kwa muda kutokana na baadhi ya wachezaji na makocha kukutwa na ugonjwa huo.
Miongoni mwa
Kocha ambaye amekuwa wa kwanza kungudulika na ugonjwa huo nchini Uingereza ni
Mikel Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal ambaye alikuwa anajiandaa kuingoza timu yake
kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Brighton ambao nao umeahirishwa.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti makocha hao ambapo Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons,
Adolf Rishard amesema kuwa amekuwa akifuatilia mwenendo wa habari zinazohusu
Corona jambo ambalo linashtua dunia nzima licha ya kwamba haujafika Bongo kuna
umuhimu wa kuomba lisifike na wagonjwa wapone.
“Kwa sasa
imekuwa ni tishio la dunia nzima kwani wahanga ni binadamu wenzentu na kwenye
familia za michezo tunaona namna hali ilivyo, maombi yetu ni kuona kwamba
ugonjwa huu hautui Bongo na kwa wale ambao wanaumwa tunawaombea wapone ili
maisha yaendelee,” amesema.
Hitimana Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa ni aina ya ugonjwa ambao una kasi kwenye kupunguza nguvu kazi licha ya kwamba haujafika Tanzania kuna umuhimu wa kuomba na kuzingatia kanuni za afya ili kujikinga na virusi hivyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment