SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kuna shindani mkubwa wa namba ndani ya kikosi chake jambo linalompasua kichwa kuwapa nafasi wachezaji wake.
Raia huyo wa Ubelgiji amesema kuna wachezaji ambao wamekuwa wakikosekana uwanjani licha ya kuwa na uwezo mkubwa ila anashindwa kuwatumia kutokana na kubanwa na idadi ya wachezaji ambao wanahitajika kutumika ndani ya kikosi cha kwanza.
"Kuna wachezaji wengi wazuri ndani ya timu na kila mchezaji anahitaji kucheza jambo hili linanifanya niwe kwenye hesabu kali za kujua namna gani nitawatumia wote.
"Ninajua watapata nafasi ya kucheza kwa kuwa wanahitaji kucheza lakini wanapaswa waongeze juhuhudi pale watakapopewa nafasi ya kucheza," amesema.
Miongoni mwa wachezaji ambao hawaonekani mara kwa mara uwanjani ni pamoja na Shiza Kichuya, Ibrahim Ajibu, Said Ndemla, Rashid Juma, Yusup Mlipili.
Ajibu atasugua sana tu benchi mana ni goigoi wa mazoezi ndo mana aliikataa offer ya kwenda TP mazembe.
ReplyDeleteKichuya sijui nani alimdanganya kurudi soka la bongo vigisu vingiiiii bora kaka ungebakia huko huko tuuuuuu, naamini umejifunza. Kitakachofata utatolewa kwa mkopo kwenda Ndanda , singida united au Mbao.
ReplyDelete