March 15, 2020


NYOTA wa timu ya Yanga, Haruna Niyonzima amesema kuwa sababu kubwa iliyomfanya asijiunge na kikosi cha Yanga ambacho leo kitacheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC ni kadi zake tatu za njano alizopewa kwenye mechi alizocheza.

Niyonzima amesema kuwa hajagoma kuendelea kuitumikia n Yanga kama ambavyo inaelezwa kwani yeye ni mali ya Yanga.

"Inaelezwa kuwa nimegoma kuitumikia timu yangu hiyo sio kweli bado ni mali ya Yanga ila nimeshindwa kujiunga na wenzangu kutokana na kuwa na kadi tatu za njano," amesema.

Niyonzima amekuwa akitimiza majukumu yake ndani ya Yanga ambapo kwenye mechi zote mbili dhidi ya mabosi wake wa zamani Simba alionyesha balaa lake ndani ya dakika zote 180.

4 COMMENTS:

  1. Hamna lolote ni kipigo tu leo! Mimi nimehamia Simba mapema sasa!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huna jipya wewe c mwanajangwani,kujibadili sura wakat moyo ni ule ule ni uboya wewe

      Delete
  2. Wewe uliporudi kwa timu yetu Yanga uliahidi umerejea kuipa ubingwa basi tnaungoja ubingwa uliahidi na ya he kuigomea jambo ambalo umelizoea na hata pale ulipokueepo kwa watani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic