March 2, 2020


UONGOZI wa Simba umesema kuwa utaanza kuipigia hesabu Yanga baada ya kumalizana na Azam FC  kwenye mchezo wao wa Ligi utakaochezwa Machi 4, Uwanja wa Taifa.

Machi 8, Uwanja wa Taifa, Simba itamenyana na Yanga  kwenye mchezo wa pili wa mzunguko wa pili ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandnbroek, amesema kuwa hesabu zake kwanza ni kwa mechi yake ya Azam kisha akimaliza hiyo itafuata dhidi ya Yanga.

"Mpango wa kwanza ni Azam kisha baada ya hapo tutamalizia na Yanga, natambua utakuwa mchezo mgumu ila acha kwanza tumalizane na Azam FC," amesema.


5 COMMENTS:

  1. Mechi ya raundi ya kwanza Simba na Yanga mashabiki wa Simba walibaki kuwalaumu wachezaji wa Simba na kocha wao lakini nje ya uwanja mashabiki wa Yanga na viongozi wao walifanya juhudi kubwa kiftina kuhakikisha wanashusha moral za wachezaji wa Simba ndani ya uwanja. Kama mdau wa mnyama nawasihi mashabiki wenzangu wa Simba kuzichukulia hizi mechi mbili kati ya Azam na Simba na Yanga na Simba kama ni mechi za ubingwa. Kwa upande wa uongozi wetu wa Simba tunashauri ingekuwa vizuri wachezaji wakawekwa kambini ili kuwapa wachezaji utulivu. Kwa wachezaji wa Simba wafahamu kuwa wamekuwa wakijitoa vya kutosha kuipigania timu ila kunako mechi hizi mbili za Azam na Yanga wanatakiwa kuutetea ubingwa na uwezo huo mnao kwani mechi hizi mbili hasa ya Yanga ni mechi zaidi ya ubingwa. Kwa upande wa kamati za fitna za Simba ni kuhakikisha Yanga anapoteza zidi ya mbao. Yanga ni timu isio na pumzi hasa kipindi cha pili na uwezekano wa kucheza mchezo wa kupaki basi zidi ya Simba ni mkubwa kwa hivyo nnaimani benchi letu la ufundi halitarejea makosa ya mechi iliopita.kwa upande wa TTF tunaomba kuteua waamuzi wenye uwezo wa kutosha zidi ya mechi hizi kubwa kuepusha haki kutotendeka. Ni mechi zinazowahusisha viongozi wa ligi na wanaomfuatia kwa hivyo utaona kwa kiasi gani ushindani wa mechi utakuwa.

    ReplyDelete
  2. FITNA NI JAMBO LA KAWAIDA BHANA,MBONA HATA MBELE WANAFANYA FITNA CHA MSINGI NIKUJIANDAA KISAIKOLOJIA KWA UPANDE WA WACHEZAJI MAANA HILI HALIWEZI KUEPUKIKA,JAPO BADO YANGA ANA KIBARUA KIZITO KUJINASUA MBELE YA MNYAMA MWENYE HASIRA NA NJAA KALI YA USHINDI,SIMBA IKO SAWA JAPO MAPUNGUFU KWA KILA TIMU NI KITU AMBACHO TIMU ZETU HAZIWEZI KUEPUKA,NA TUMEONA KWA LIGI YETU SIMBA PEKEE NDIO TIMU YENYE NAFUU KWAKUZINGATIA TAKWIMU 1:KWANZA INAONGOZA LIGI,2:IMERUHUSU MAGOLI MACHACHE NA INAONHOZA KWA CLEAN SHEETS,3INA ALAMA NYINGI KWAKUTOKURUHUSU KUPOTEZA MECHI NYINGI,4:IPO KATIKA MOTO WA MWENDELEZO WA USHINDI(PSYCHOLOGICAL STATE OF MIND) JAPO SIO KIGEZO CHA MSINGI,5:MAINGIZO MAPYA YA SIMBA YANAZID KUONYESHA UWEZO WA HALI YA JUU HATA WEWE UNAESOMA NI SHAHIDI WA HILI,NIFUNGE TU KWAKUSEMA MAANDALIZI NI MUHIMU KWA TIMU ZOTE(MIND SETING) KWA LENGO LA KAMA SI KUZUIA BASI KUPUNGUZA MADHARA AMBAYO YANGEWEZA KUTOKEA AU YANAWEZA KUTOKEA,POVU RUKSAAAAAAA.

    ReplyDelete
  3. Mpira wa kiswahili utaishia hivi hivi

    ReplyDelete
  4. Simba ni Timu yenye malengo ya next level sitegemei ishindwe kucheza mpira mkubwa kisa fitina za kibongo. Naamini tuta burudika vya kutosha angalizo wenye moyo mwepesi wajikaze zaidi, mpira ni mchezo wenye matokeo ya kikatili, tusiende na matokeo yetu mifukoni.

    ReplyDelete
  5. nadhani kila timu ichukulie kama timu zingne tu maana naona ni point tatu kila timu ikicheza bila ya pressure nadhani tutaona mpira mkubwa sana ingawa kwa simba ina kibarua cha pekee maana wanawababe wawili, ambao ni azm na yanga na wote wanawania ubingwa alichafanya simba kushusha pressure ni kupiga mahesabu ya gap kubwa la point hapo ndo kuna uafadhali lakini lazima mpira uchezwe kwan tumeshuhudia mechi nyingi sana nadhani hata hii itapita na maisha yataendelea

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic