KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Said Ndemla ambaye amekuwa adimu uwanjani kutokana na ushindani wa namba ndani ya kikosi hicho amesema kuwa bado yeye ni mchezaji wa Simba.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ndemla amesema kuwa ana maelewano mazuri na Kocha Mkuu wa sasa, Sven Vandernbroeck aliyechukua mikoba ya Patrick Aussems aliyechimbishwa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu.
Simba kwa sasa ina viungo wengi ikiwa ni pamoja Said Dilunga, Ibrahim Ajibu, Francis Kahata na Sharaf Shiboub ambapo Sven amesema kuwa nafasi ya mchezaji kuanza inatokana na juhudi zake.
“Bado nipo ndani ya Simba na sijajua ishu yoyote kuhusu kuondoka kwangu ndani ya Simba na ninazidi kupambana ili kupata nafasi ya kucheza kwani suala hilo halipo mikononi mwangu ni suala la kocha.
“Kuna program ambayo nimepewa na kocha muda huu wa mapumziko ili kulinda kipaji changu ninaamini nitarejea kwenye ubora,’ amesema Ndemla.
Ndemla amecheza mechi tatu sawa na dakika 270 kati ya mechi 28 ambazo zimechezwa ambapo alicheza dakika 90 mbele ya Biashara United 90 mbele ya Singida United enzi za Aussems na wakati wa Sven amecheza dakika 90 mbele ya Ndanda.
0 COMMENTS:
Post a Comment