March 24, 2020



 KOCHA wa zamani wa Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino  anatamani kuona siku moja anarejea katika klabu ya Newell's Old Boys  akiwa na staa wa Barceona Lionel Messi.
 Pochettino ambaye ni raia wa Argentina aliwahi kuichezea klabu hiyo wakati anaanza soka kama ambavyo Messi  naye ameanzia soka katika klabu hiyo.
“Matumaini yangu ni kuona siku moja narejea katika klabu ya Newell's Old Boys  naona kama nachelewa  lakini itakuwa ndani ya miaka 10 ijayo, ila nitakuwa na Messi.
 Pochettino  alisema kuwa matumaini yake makubwa yako hivyo lakini anaamini kuwa  Messi atacheza hata Kombe la Dunia lijalo.
“Messi atacheza Kombe la Dunia Qatar 2022 na  atafanya vizuri bila kujali umri wake atapambana tu, unajua uwepo wake ndani ya timu ni kitu kikubwa sana ataipambania tu Argentina kwenye michuano hiyo," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic