March 4, 2020


SIMBA leo imemalizana na Azam FC kwa ushindi wa mabao 3-2 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Azam FC iliyo chini ya Arstica Cioaba ilianza kuzifumua nyavu za Aishi Manula dakika ya 4 kupitia kwa Nevere Tegere na iliwachukua dakika nne Simba kurekebisha makosa yao kupitia kwa Erasto Nyoni.

Dakika ya 14 Deo Kanda aliongeza msumari wa pili na kuifanya Azam FC kwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao moja huku Simba ikiongoza.

Kipindi cha pili Azam FC walikuja kwa kasi na kuweka mzani  sawa dakika ya 49 kupitia kwa Idd Seleman 'Naldo' na kufanya ngoma iwe 2-2.

Meddie Kagere alikuja kuweka usawa kwa Simba ambapo alifunga bao la ushindi dakika ya 72 ambalo lilipa pointi tatu Simba.

Obrey Chirwa dakika ya 83 alipachika bao matata baada ya Manula kutema shuti la Richard Djod ila mwamuzi alitafsiri kuwa aliotea.

Ushindi huo unaifanya Simba ifikishe jumla ya pointi 68 kibindoni ikiwa nafasi ya kwanza na Azam FC inabaki na pointi 48 zote zikiwa zimecheza mechi 26.

8 COMMENTS:

  1. Penati 2 na bao la offside=Azam kuonewa

    Simba=Goli la Kagere krosi ya kapombe mpira uko nje Je ni Utata?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi kwa nini na nyie msijifunze urefarii mkapewa hizo beji za FIFA?Nini kinachowazuia? Msiwahukumu marefarii kwa mahaba yenu kwa timu zenu.Ikiwa hizo VAR nazo zinalalamikiwa sembuse binadamu.

      Delete
  2. Tujadili pia mpira mzuri wa kuburudisha wa simba, was fantastic, simba walikuwa wamalize mchezo kipindi cha kwanza

    ReplyDelete
  3. wewe refa uliona mpira uliokwenye chaki umetoka

    ReplyDelete
  4. Walisema hivyo hivyo nä Pyramids ohh mpira umetoka Ngassa akauruka kuja kugeuka watu wanarudi .Mpira utoke lazima utoke wote. Ujinga wa kudhani ni ujinga usio na sababu.Cha ajabu Azam hawalalamiki anayelalamika ni Kwasukwasu.Punda wa nyuma hajaguswa lakini ndio anayepiga mayowe. Maajabu.

    ReplyDelete
  5. Hao vyura matopeni wanaanza vioja vyao utafikiri wao ndio watete I wa haki, a binaadamu wa asahau kuwa wao wenyewe hali tete baada ya kuangamiza mabilioni ya watu kuninulia magarasa. Wacha cheza na MOOOOO

    ReplyDelete
  6. .mmesahau goli la lipuli mkasema mpira haujavuka mstar, sjui mipira ya Simba ndio inakua inatoka hata Kama ipo kwenye chak,? dah wabongo bhana, pia polis Tanzania goli la Waz wakakataa hapo hamlamiki au mkuki kwa nguruwe kwa binadam mchungu, ebu tushbir tar 8 kila mtu ashangilie tm yake

    ReplyDelete
  7. Bado sana watafungwa sana kwa ujinga wao na mwisho wa siku kombe linakwenda msimbazi,yanga jipangeni upya acheni kulalama mnazidi kujiaibisha mjue.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic