JOHN Bocco, nahodha wa Simba amesema kuwa kilichowaponza kushindwa kusepa na pointi tatu jana Machi 8,2020 mbele ya Yanga ni kutokuwa makini kuzitumia nafasi walizotengeneza.
Simba ilichapwa bao 1-0 na Yanga kwenye mchezo wa mzunguko wa pili na kuifanya iache pointi tatu zikisepa jumla kwa Yanga Uwanja wa Taifa.
"Haikuwa kazi nyepesi kwani tulipambana kupata matokeo mambo yakawa magumu kwetu, wapinzani wetu walikuwa vizuri na walitumia nafasi moja waliyoipata tofauti na sisi tulishindwa kuwa makini kuzitumia nafasi tulizozipata.
"Tunajua hali ya mashabiki ilivyo hata sisi pia hatujapenda kupata matokeo haya ila tunawaomba waendelee kutupa sapoti kwani mechi bado zipo nyingi tutafanya vizuri," amesema.
Simba inabaki kuwa nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 27 ikiwa na pointi 68 kibindoni huku Yanga ikiwa nafasi ya tatu na pointi 50 ikiwa imecheza mechi 25.
Ki ukweli pamoja na kwamba mpira una matokeo 3 ila wachezaji wa simba walicheza kibishoo sna pia benchi la ufundi waangalie vizur timu haina viziki kabisa pia nadhan jana mkude alikuwa na jambo kichwan kwake ika ajue simba ni timu kubwa ina fans wengi staki kumuhukumu ila ile ni daby ningetaman kumwona mkude anapambana ka tshishimbi au makapu hapa sizungumzii rafu iliyozaa goli ila ile rafu nyingine ingekuwa refa kutoka nje ni umeme now tumekubali matokeo simba nguvu moja
ReplyDeleteNi kujifunza tu. Kocha alikuwa anatakiwa afahamu mapema kipindi cha kwanza ya kuwa game plan ilifeli ila amekuja kubadili mfumo dk 15 za mwisho. Kuna wakati unacheza na forward mmoja na mwengine unacheza na wawili yote inategemea hali ya mchezo. Yote kwa yote tunaweza kukutana tena FA cup.
DeleteSimba ilionyesha kuwa haikua na nguvu ya kupambana mwanzoni na maoni yangu ni kuwa hilo lilisababishwa na kuwa imetoka kucheza mchezo mgumu na Azam equally wa upinzani mwanzo mwisho kama wa Yanga. Na ndani ya siku mbili miili ya wachezaji ilibaki bado na mchoko wa wazi kabisa kuanza tena kupambana kwa kasi ile ile kama mchezo uliopita. Hata hivyo nawapa pongezi kuweza kurudi na kupambana, na haikuwa bahati yao jana kwani walipata nafasi nzuri za kushinda labda hata kuliko Yanga ndio mpira.
ReplyDeleteKuhusu ratiba hata mimi nimeshangazwa pia. Yaani baada ya dabi tu kuna mechi jumanne na Singida Utd wakati mwenye viporo viwili hana mechi mpaka alhamisi.
DeleteWachezaji walionekana wamechoka mapema kabla ya mechi goli la kijinga tumefungwa basi bingwa ni mnyama tu hilo halina ubishi
ReplyDeleteInaelekea kuna comment hamtaki zitokee, bas mngeelekeza mnataka tu za mlengo wenu mueleze mlengo up.
ReplyDeletesimba .drop it and get own serengeti ni yenu ...
ReplyDeleteWhere is my publised comment! why does it not remain for others to see the other side of view.
ReplyDeleteKwanini mnafuta baadhi ya coments??
ReplyDeleteLabda kama kuna lugha isiyo ya kiungwana imetumika ila humu sijawahi kupata shida ya kupost comments
DeleteSimba inabidi tubadilike sana kama mwakani tunataka kufikia level za Tp mazembe na Mamelod Sundown.Ukiangalia timu yetu upande wa golikipa, namba nne na namba tano inabidi benchi la ufundi wafanye mabadiliko haraka sana.Manula, Kakolanya siyo makipa wazuri inabidi tutafute makipa Level za wakina Mwameja.Nyoni na Wawa umri umewatupa mkono.
ReplyDeleteSasa kilichotuponza jana ni kwamba kocha alipanga kikosi cha kufurahisha mashabiki, namaanisha Kagere na Bocco mmoja alitakiwa aanzie bechi halafu Deo Kanda na ile speed yake awasumbue Yanga.Ila yote ni mchezo wachezaji walijitahidi lakini bahati haikuwa yetu, ingawa ni goli la kipuuzi la Jonas Mkude.Tujipange kwa game zinazokuja ili tutetee ubingwa wetu
Boko anaongea sana kuliko vitendo yeye anastahili lawama kwa kutokuwa mchezoni na kupoteza nafasi nyingi na sio game na yanga takribani game tatu zilizopita amekuwa chini ya kiwango
ReplyDelete