March 2, 2020

IMEELEZWA kuwa kinachoiponza Mwadui FC kushindwa  kuwa na mwendelezo mzuri wa matokeo ndani ya Ligi Kuu Bara ni hali ngumu ya kiuchumi ambayo wanaipitia kwa sasa.

Mwadui FC ilikuwa timu ya kwanza kuitungua Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanjawa Kambarahge kwa kuifunga bapo 1-0 lililofungwa na Gerald Mdamu.

Habari zinaeleza kuwa wachezaji wengi wanadai stahiki zao jambo ambalo linawafanya wacheze wakiwa na mawazo mengi kuhusu ishu ya mkwanja na gharama za maisha.

"Mwadui ilikuwa imara ila imeshindwa kudumu kwenye uimara wake kutokana na wachezaji kudai stahiki zao, wengi hawajalipwa na wanaendelea kufanya kazi jambo hilo linaua morali ya wachezaji hivyo ndio maana hakuna mabadiliko makubwa zaidi ya kusasua tu," ilieleza taarifa hiyo.

Meneja wa Mwadui FC, David Chakala amesema kuwa huwa wanawaambia wachezaji wao kuwa mpira ni kazi yao wanapaswa waitimize ilikufikia malengo waliyojiwekea.

Mwadui FC ipo nafasi ya 16 imejikusanyia pointi 25 baada ya kuecheza mechi 24.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic