DAKTARI wa Yanga, Sheikh Mngazija, amewapangia wachezaji hao vyakula maalumu na kuwapiga stop wachezaji hao kula vyakula visivyoeleweka.
Agizo hilo limetolewa na daktari huyo kutokana na kuhofia wachezaji hao kujiachia kwa kula vyakula ambavyo vinaweza kuwaongezea kilo nyingi katika kipindi hiki ambacho wapo majumbani kwao.
Akizungumza na Championi, Mngazija alisema kuwa amewakataza wachezaji kula vyakula kama chipsi mayai na vyakula vingine vingi vyenye asili ya mafuta kwa ajili ya kuhofia kuongezeka uzito.
“Niliwapa maagizo ya kuchagua baadhi ya vyakula ili isije kuwaletea shida pindi watakaporejea maana wakitumia vyakula vyenye asili ya mafuta kwa wingi kama chipsi au mayai na vingine itakuwa si njema kwa afya yao kwani wanaweza kuongezeka kilo au unene tofauti na walivyokuwa mwanzo.
“Unajua wachezaji wanapokuwa kambini ni tofauti na wanavyokuwa majumbani kwao kwani wakiwa kwao wanaweza wakafanya vyovyote lakini kuhusu vyakula nimejitahidi kuwapa onyo na kuwasihi wale vyakula vitakavyowafanya wapate nguvu kama vyakula vya wanga,” alisema dokta huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment