March 26, 2020


CORONA kwa sasa imekuwa ni janga la dunia kiujumla kutokana na kusababisha athari kubwa kwa jamii ambayo ndani yake kuna familia pia ya wanamichezo ambayo kwa sasa imepoteza furaha yake ya muda.
Virusi hivi ambavyo vinasababisha ugonjwa wa COVID-19 vinaitikisa dunia ambayo inahaha kutafuta suluhisho lake ili kurejesha amani ambayo kwa sasa imetikisika.
Katika haya yanayotokea tunaona Serikali imeamua kulivalia njunga suala hili kwa kujali usalama na maisha ya raia wake ambayo ni muhimu .
Tunaona suala la michezo  kwa sasa imesimama kwani wakati Ligi Kuu Bara inaendelea watu wengi walikuwa wakikutana viwanjani kwa ajili ya kushangilia timu zao ila kwa sasa hali hiyo haitaendelea.
Agizo la Serikali lina afya ndani yake kwani kwa kufanya hivyo kumewafanya watu wake kuwa salama na kuendelea kupambana na Virusi hivi ambapo kwa wale waliokutwa na tatizo hili wanapewa huduma huku wakiwa wamewekwa kwenye uangalizi maalumu.
Waziri mkuu, Kassim Majaliwa, Machi 17 alizuia masuala yote ya mikusanyiko isiyo ya lazima na kusimamisha shughuli zote za michezo kuanzia Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi ya Wanawake.
Tunaona kwamba shule na vyuo pia vimefungwa kwa muda ili kupita kwenye kipindi hiki cha mapambano dhidi ya Corona ni lazima taifa liungane na kuongeza nguvu kwenye mamapambano ya Virusi.
Afya ni kitu cha msingi kwa wana familia ya michezo pia kwani wale ambao walikuwa wakisumbuliwa na magonjwa wakati ule ligi ikiendelea ilikuwa ni nadra kuwakuta viwanjani.
Kwa sasa napenda kuwaambia watanzania kuwa ni muhimu kuchukua tahadhari na kufuata yote ambayo yanashauriwa na wataalamu wa afya pamoja na Serikali ili kujikinga na Virui hivi.
Kitu cha msingi ni kutambua kwamba ugonjwa huu upo na ni wa hatari kwani yule ambaye atapuuzia itakuwa ni makosa makubwa hasa kwa wakati huu ambao kila mmoja anapambana kuona namna gani tunaweza kuvuka tatizo hili.
Kikubwa kinachotakiwa ni kufuata masharti ambayo yamewekwa na kuwa makini katika kila hatua tunayopitia kwa sasa huku tukiamini kwamba wakati wa tatizo hili kuisha unakuja.
Chama cha mpira Tanzania (TFF) kimekuwa bega kwa bega na Serikali ambapo kwa kulitambua hilo kimesema kuwa iwapo ligi itaanza  mashabiki hawatapata nafasi ya kuibukia uwanjani.
Kwa mujibu wa Almas Kasongo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania alisema:” Kulingana na hali halisi ya kuunga mkono juhudi za Serikali kupambana na Corona, basi endapo ligi itaanza hakutakuwa na mashabiki ndani ya uwanja ili kupunguza maambukizi,”.
Katika hilo bado ninaunga mkono kwamba Bodi ya Ligi Tanzania imetazama umuhimu wa afya za watazamaji na ukubwa wa tatizo lilivyo hapo ni lazima kuheshimu maamuzi.
Hali ni ngumu natambua kwamba kuna wale ambao wataamua kuonyesha kwenye vibanda umiza katika hili pia ni muhimu kutumia busara na tahadhari kubwa hasa kwenye mkusanyiko wa watu.
Ninachoamini mimi kuna umuhimu pia wa wamiliki wa vibanda umiza kulitambua hili na kulichukulia katika uzito isije kuleta matatizo kwa jamii hapo baadaye.
Tusidharau hili ni jambo la msingi na mumimu kuchukua tahadhari muda wote bila kujali upo maeneo ambayo upo kwa wakati huu tuliopo afya iwe kipaumbele cha kwanza na kila mmoja awe mlinzi wa mwingine.
Suala la mashabiki kuzuiwa kuingia viwanjani hili suala halipo kwetu pekee bali dunia nzima huwa inatokeoa mwisho wa siku watu wanaeelewa nini ambacho kinatakiwa kifanyike na kinafanyiwa kazi.
Tukiachana na suala la tahadhari kwa wachezaji nao wasijisahau muda huu wanapokuwa nyumbani wakisubiri ligi kurejea ndipo wakamilishe ile lala salama ambayo ilikuwa imebaki.
Kila timu inatambua nafasi yake iliyopo na hali halisi ilivyo ni muhimu kila mmoja kufanya kazi yake kwa umakini ili kupata matokeo mazuri.
Mwezi huu mmoja  wa mapumziko watumie kurekebisha makosa yao ambayo waliyafanya kwenye mzunguko wa pili na ule wa kwanza ili kuwa kwenye ubora wao.
Ligi ikianza bila mashabiki tutaona kwenye tv ambapo Azam TV wamekuwa wakionyesha mechi nyingi za Ligi Kuu Bara.
Kwa wale ambao watakuwa wamezembea kufanya mazoezi na kujipanga kwa usawa itakuwa ngumu kwao kujinasua pale walipo na kujikuta wakiishia kwenye shimo ambalo hawakuritarajia.
Muhimu ni kujipanga kwa ili kupata kile matokeo chanya ambayo yaafanya timu kuwa pale ambapo zinahitaji kufika na kikubwa ni kuona kila mechi inakuwa na matokeo tofauti na yale yaliyopita.
Kuna timu ambazo zimeshajifungia ukurasa wao ndani ya ligi kutokana na kutokuwa na mwendo mzuri ndani ya ligi jambo hili ni baya iwapo zitaamua kuwa daraja la kufungwa kwenye mechi zao zilizobaki kwa kutengeneza matokeo.
Hili linavunja hali ya ushindani na kufanya wachezaji kutokuwa na maadili ama yule anayecheza mchezo wa kupanga matokeo kutokuwa na uadilifu ambapo utawafanya waepuke masuala ya kupanga matokeo.
Nje tunaona mtu wa mwisho anakaza na kumtandika yule aliye ndani ya tano bora hata kiongozi wa ligi anachapwa kutokana na ushindani na hili linatakiwa pia kwenye ligi yetu ya Bongo.
Kwa kufanya hivyo kutasaidia ushindani kuwa mkubwa na kila mmoja kufanya majukumu yake kwa wakati bila ujanjaujanja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic