ALLIANCE FC
iliyo chini ya Felix Minziro kwa sasa inasumbuka na msala walioachiwa na
washambuliaji wa Yanga ambao ni David Molinga na Patrick Sibomana baada ya
kuitungua mabao 2-0 Uwanja wa Taifa, Februari 29.
Baada ya
kichapo hicho Alliance imecheza mechi tatu ambazo ni sawa na dakika 270 bila kuambulia bao zaidi ya kufungwa mabao
matatu na kupoteza pointi tisa.
Machi 3, Alliance ilipoteza mchezo wake
uliochezwa Uwanja wa Mabatini, kwa kufungwa na Ruvu Shooting bao 1-0. Machi 7, ilichapwa bao
1-0 mbele ya Azam 1-0 na Machi 11 ilichapwa bao 1-0 mbele ya Tanzania Prisons.
Leo itakuwa na kibarua
kingine mbele ya KMC iliyo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 30 huku Alliance ikiwa
nafasi ya 18 na pointi 29 zote zimecheza mechi 28.
0 COMMENTS:
Post a Comment