HATIMAYE ukarabati wa Uwanja wa Azam Complex, umekamilika kwa asilimia 100.
Uwanja huo ulikuwa unafanyiwa ukarabati ambapo nyasi zote zilifumuliwa na kuanza kuwekwa upya kabisa na inaelezwa kuwa zaidi ya bilioni tatu zimewekwa chini.
Wakati wa maboresho Azam FC walikuwa wanatumia uwanja wa Uhuru na Taifa kwenye mechi zao za nyumbani sasa watarejea Chamazi.
Iwapo Ligi Kuu Bara itarejea hivi karibuni kutokana na kusitishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona basi uwanja wao utakuwa wa Chamazi.
Ni miongoni mwa viwanja bora Afrika vilivyowekwa nyasi za kisasa kabisa za bandia ukiachana na Azam Complex ni pamoja na ule wa TP Mazembe (Stade TP Mazembe) ya Congo.
0 COMMENTS:
Post a Comment