April 12, 2020


 HAKUNA anayejua kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara itarejea lini kwa msimu huu wa 2019/20 kutokana na kusambaa kwa Virusi vya Corona.
Hii inatoa nafasi kwa wachezaji kuendelea kuwa mabalozi wakiwa nyumbani wakisubiri tamko la Serikali kuruhusu yake ambayo waliyakataza.
Ninaona kwamba kuna wachezaji ambao wamekuwa wakionyesha jitihada za kufanya mazoezi kulingana na program ambazo walikuwa wamepewa na benchi la ufundi.
Muhimu kwao wanatakiwa kufuata yale ambayo wamepewa wakati huu ili kutimiza yale ambayo wanatakiwa kuyafanya kwa muda huu ambao ligi imesimama.
Ikitokea kila mchezaji akafuata program ambazo amepewa itawarahisishia benchi la ufundi pale ligi itakapoanza kuendelea na kasi ambayo walikuwa nayo awali.
Iwapo wachezaji watashindwa kuelewa wanachotakiwa kukifanya dunia imekuwa rahisi hasa kwa upande wa mawasiliano ambapo wanaweza kuzungumza mojakwamoja na kocha wao ambaye atakuwa akiwasimamia.
Tunaona kwama mbinu ambazo zinatumika na timu nyingi duniani ni kupitia mitandao ambapo wachezaji wanawasiliana na wachezaji wenzao pamoja na benchi la ufundi mojakwamoja.
Hii ni sawa kwani mazingira yamekataa kuwaona wachezaji wakiwa pamoja baada ya maambukizi ya Virusi vya Corona.
Hili ni agizo ambalo linapaswa lifanyiwe kazi hakuna ambaye anapaswa ajitokeze kwenye mikusanyiko ya wengi ambayo inatokea iwapo hakuna umuhimu.
Tahadhari inabidi ichukuliwe na kila mmoja kwenye kazi yake anayoifanya ili kujilinda kwa kuwa anatakiwa kuwa salama muda wote.
Serikali inahitaji kuona watu wake wakiwa salama ndio maana iliamua kusimamisha masuala yote ambayo yalikuwa yanakusanya watu ili kupunguza msongamano wa watu kwenye sehemu ambazo hazina ulazima.
Kwa kiasi chake  ninaona wazazi wameanza kuelewa kuhusu umuhimu wa kuwalinda watoto hii ni sawa na inafurahisha kwa kuwa tunakuwa tunaunga mkono juhudi za Serikali.
Iwapo kila mmoja ataendelea kuchukua tahadhari itatoa fursa kuweza kuitokemeza Corona kwa kiasi chake na hatimaye itatuacha salama nasi tutaendelea kufanya kazi kama zamani.
Ukubwa wa tatizo ambao upo kwa sasa ni lazima uendane na kasi ya kufuata kanuni za afya ambazo zinatolewa kila siku na Serikali pamoja na Wizara ya afya.
Bado napenda kuwasisitizia wachezaji wasiache kufuata kanuni za afya na maelekezo waliyopewa na makocha wao imani yangu inaniambia kuwa wanapaswa wawe tayari muda wowote wakishindwa kulinda viwango vyao wataanza upya.
Ligi Kuu Bara itakaporejea inakuwa ni wakati wa kukamilisha mzunguko wa pili huku kila timu ikiwa inatambua kile ambacho inakihitaji ndani ya ligi.
Kuna zile ambazo zitarejea kwa ajili ya kutafuta ubingwa kwa kuwa zipo kwenye afasi nzuri ya kufikia malengo hayo kutokchagi wakimaliza la na mechi ambazo wanazo.
Pia zipo ambazo zenyewe hazina haraka ya kujiweka kwenye ubingwa bali zinajiweka ndani ya kumi bora hili nalo linaongeza ushindani kwenye ligi.
Ikumbukwe kuwa zinashuka timu nne msimu huu huku zile mbili nyingine zitacheza playoff hii itafanya iwapo mambo hayatakiwa  magumu kwa timu ambazo zinatakua kwenye nafasi ya 15 na 16 kujikuta zikiibukia ndani ya Ligi Daraja la Kwanza.
Hapo unaona kwamba ni lazima kila timu ipambane kupata matokeo mazuri pale ligi itakapoanza ili wappate matokeo mazuri yatakayowafanya wabaki ndani ya Ligi Kuu Bara.
Uzembe wa wachezaji usiwe kigezo kwa timu kuporomoka kutoka kweye mfumo ambao walikuwa nao hapo awali haitapendeza.
Ukweli ni kwamba kwa namna yoyote ile mchezaji ambaye hatapata muda wa kufanya mazoezi hata yale ya kukimba atakuwa na kazi kubwa kwenye kikosi chake kurejea kwenue ubora wake.
Itakuwa kazi kurejea kwenye ubora iwapo hafanyi mazoezi na huenda inaweza kuwa baada ya kucheza mechi tano hata sita lakini utakuwa muda umwekwenda kutokana na mzunguko wa pili kubakiwa na mechi chache.
Kwa wale ambao wanaendelea na mazoezi nyumbani ninapenda kuwapa pongezi hii ni kazi ambayo inahitajika kujisimamia wenyewe na ni ngumu.
Ninatambua kwamba kiasili wengi ni wajanjawajanja linapofika suala la kufanya mazoezi wanadhani wanaikomoa timu wanasahu kwamba ni kazi yao lazima wafanye.
Ili wawe katika ubora na ushindani ni lazima waendelee na mazoezi itawasaidia kuwa kwenye ubora ambao walikuwa wameishia wakati ligi inasimamishwa.
Mashabiki pia ni muhimu kuwa na subira kwa wakati huu pamoja na kuchukua tahadhari kulinda afya zao ambazo ni muhimu kuona namna gani kila mmoja atakuwa salama.
Afya za mashabiki ni muhimu pia katika hili hivyo ili kuwa bora katika ushangiliaji wakati ujao ni muhimu kulinda afya zao na kujiepusha na mikusanyiko isiyo ya lazima.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic