April 24, 2020


SELEMAN Matola ndani ya Simba msimu huu ameongoza timu hiyo kwenye mechi 18 akiwa ni Kocha Msaidizi baada ya kujiunga na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara akitokea Polisi Tanzania.

Ameshuhudia JKT Tanzania na Yanga zikisepa na pointi sita mazima baada ya kupoteza mechi hizo kwa kuambulia kichapo cha maana.

JKT Tanzania ilimtungua Beno Kakolanya bao 1-0 Uwanja wa Uhuru na Yanga ilimtungua Aishi Manula bao 1-0 Uwanja wa Taifa.

Matola akiwa benchi pia ameshududia wakigawana pointi moja na Yanga Uwanja wa Taifa kwa sare ya kufungana mabao 2-2.

Tabasamu lake lilionekana kwenye mechi 15 ambapo walisepa na pointi 45  mazima baada ya kushinda kibabe ndani ya ligi.

Akiwa kwenye benchi ni Yanga wamempa tabu kubwa msimu huu tofauti na msimu uliopita alipokuwa Lipuli ambapo aliwabana mbavu kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho msimu huu hajapata bahati ya kusepa na pointi tatu kwenye timu zote mbili.

Alipokuwa Polisi Tanzania alikubali sare ya kufungana mabao 3-3 na kugawana pointi moja na alipoibukia Simba ameambulia pointi moja na moja amechapwa.

Hatimaye leo anaongeza miaka kadhaa, heri ya kuzaliwa Seleman Matola.

5 COMMENTS:

  1. Uandishi wa kipuuzi kabisa. Shida yako nini hasa, kutujulisha juwa matola leo ni birthday yake au kutangaza kuwa yanga alimfunga simba?

    ReplyDelete
  2. Upuuzi mtupu. Hawa waandishi uchwara tuwapuuze tu.Eti kichapo cha maana?Gepu la pointi 21 bado haliwatoshi.Gongo wazi na waandishi wao .Mwadui, Yanga na JKT wamechukuwa ubingwa kwa kuifunga Simba,?Reasoning ya kitoto haswa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Povu la nini kwani wewe ndiye Matola?Pilipili usiyoila yakuwashia nini,upuuuzi tuu

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic