UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa hauna mashaka iwapo Kocha Mkuu, Luc Eymael atapendekeza majina ya nyota wawili wanaokipiga ndani ya Simba ambao ni Deo Kanda na Clatous Chama watue jangwani.
Kanda na Chama wamekuwa wakihusishwa kutua ndani ya Yanga ambayo inahitaji kuunda kikosi cha ushindani msimu ujao.
Ofisa Uhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema kuwa muda utazunguza hasa wakati wa usajili ukifika na wanaweza kumsajili mchezaji yeyote ataye pendekezwa na mwalimu.
"Jina ambalo litapendekezwa na Kocha Mkuu, Eymael litapenya na kusajiliwa bila kujali ni nani iwe Chama ama Kanda pia mipango yetu ni kuona kikosi kinakuwa bora kwa kusajili wachezaji makini," amesema.
Chama amebakisha mkataba wa mwaka mmoja ndani ya Simba hivyo iwapo Yanga watahitaji huduma ni lazima wavunje mkataba wa kiungo huyo mwenye mabao mawili na pasi saba za mwisho.

Safi sana, hata Haji Manara wakimwitaji ruksa tuu
ReplyDeleteUwezo wenu ni kuchukua wachezaji wanaokaa benchikama ndemla au mpilipili
ReplyDeleteSajilini kutoka kwingine jamani. Kwani pesa za GSM ni kwa ajili ya wachezaji walioko Simba tu?
ReplyDeleteWanajititimua bure.Hawana ujeuri wa kusajili mchezaji anayehitajika Simba.
ReplyDelete