April 18, 2020

PETER Manyika, Kocha wa makipa ndani ya Klabu ya Yanga amesema kuwa viwango vya magolikipa wa kigeni ni vya kawaida ukilinganisha na vile vya wazawa kutokana na kile wanachokionesha wawapo uwanjani ila ni wavivu.

Manyika amesema kuwa wengi wamekuwa wakifanya sawa na wazawa jambo ambalo anaamini wanatoshana nguvu.

"Wachezaji wakigeni bado uwezo wao ndani ya ligi ni wa kawaida sawa na wazawa ila tofauti yao ni ndogo tu kujituma.

"Kinachowashinda wazawa wengi ni uvivu wa kutopenda kufanya mazoezi na kujituma zaidi uwanjani ila wakiamua wanaweza kuwa bora zaidi," amesema.

Miongoni mwa makipa ambao ni wageni na wanafanya vizuri ndani ya Bongo ni pamoja na Nurdin Barola anayekipiga ndani ya Namungo FC.

Pia kwa Azam FC yupo Razack Abarola ambaye ni kipa nammba moja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic