April 14, 2020


FREDIRICK Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa hakujua kwamba kuzungumza ishu ya kutaka kumsajili kiungo wa Simba, Clatous Chama itazua mtafuruku jambo ambalo ameamua kuomba msahamaha kwa mashabiki wa Simba na Uongozi wa Simba.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mwakalebela amesema kuwa alizungumza ishu ya Chama akitambua kuwa ni sehemu ya utani wa jadi kama wao ambavyo wanafanya jambo ambalo limepokelewa tofauti.

"Sikuwa na maana mbaya zaidi ya utani kama ambavyo wao walikuwa wakifanya utani, kwa hatua mabayo nimefikia ninapenda kuomba msamaha kwa viongozi wa Simba pamoja na mashabiki katika hili.

"Unajua sisi ni watani wa jadi sasa wao walikuwa wanafanya utani juu ya kumtaka Tshishimbi nasi pia tukarejea kuanza harakati za kuinasa saini ya Chama ila limepokelewa tofauti hatukuwa na maana mbaya ila tunaomba radhi kwa hili.

"Utaratibu kuhusu masuala ya usajili tunayatambua vema ila nilichokifanya ilikuwa ni sehemu ya maisha ya utani, nimeona Ofisa Habari wao Haji Manara amezungumza, hili ni soka na kanuni zipo wazi," amesema.

Haji Manara leo amesema kuwa Chama ana kandarasi ndefu ndani ya Simba ambayo itameguka mwaka 2021.

9 COMMENTS:

  1. Hakuna cha utani. Simba haikusema officially kwamba imezungumza nä wakala wa Tshimbishimbi nä kwamba wakala amesema amebakiza miezi 6 kwenye mkataba wake.Mwakalebela amesema kwamba amezungumza na wakala wa mchezaji mwenye mkataba mrefu.Dawa ili huu ujinga uishe ni kuwaripoti tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hujui maisjjhabya mpira ww.
      yaani povu linakutoka kwa yanga na simba!
      eti kuwaripoti, kisha ww inakupa ugali au maharagwe kwa mpira wa bongo?
      amini wiki kesho hakuna mjadala huu na wao wanaendelea na maisha yao ila ww utabaki na korosho yako.

      Delete
  2. Kila siku tunasema viongozi yanga hawana wajualo, ona sasa wameuvaa mkenge, 50m zinawahusu. Hapi hakuna uta sheria ifuate mkondo wake.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nenda kamwambie mama yako kule kijijini hana ajualo kwa kumzalia baba yako toto jinga mbumbumbu kama wewe,nyau kabisa!

      Delete
  3. Hapo hakuna utani ni kutokujua nini cha kuropoka . GSM watalipa hakuna taabu

    ReplyDelete
  4. Eti shujaa, shujaa au bumbumbu wa sheria

    ReplyDelete
  5. Ushujaa wake ni upi Salehe, au na wewe ni Gongowazi.

    ReplyDelete
  6. Gongo wazi tena ja kutupa .Mtu hajui kanuni Tanzania anaitwa shujaa. UAmekimbilia kuomba radhi. Angekomaa aone moto.

    ReplyDelete
  7. Acha matusi, mambo ya mama ysnsingiaje hapa, unadhani wengine hatuwezi kuandika matusi? Chunga sana wewe usije ukaharibu blog za watu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic