April 19, 2020


TETESI mbalimbali ambazo zimeendelea kuripotiwa kila kukicha ndani ya Yanga, ni juu ya kocha wao, Luc Eymael kuhitaji kiungo mbadala wa Papy Kabamba Tshishimbi, hali ambayo inaonekana kutomtisha na kuibariki ifanikiwe kadri iwezekanavyo.

Takribani wiki mbili sasa Yanga imekuwa ikihusishwa na kuendelea kuzama kwenye mchakato wa usajili wa kiungo wa Polisi Tanzania, Baraka Majogoro, hii ni kutokana na mapendekezo ya kocha wao, Eymael ambaye ameomba kuongeza nafasi ya kiungo mkabaji na akibainisha majina mawili akiwemo mchezaji wa kigeni.

Imeelezwa kuwa uongozi huo umeonyesha nia kubwa ya kushusha mbadala katika nafasi hiyo ambayo humilikiwa na Tshishimbi, huwezi kuamini kama amebariki kwa kuwaambia viongozi hao hata kama watataka mwingine kutoka DR Congo yeye yupo tayari kuwasaidia kumleta.

“Kumekuwa na maneno mengi sana juu ya usajili ujao, na wengi wao wamekuwa wakidhani taarifa mbalimbali zinazotolewa juu ya usajili zinaweza kuwayumbisha wachezaji wetu jambo ambalo si kweli maana mimi nimezungumza na Tshishimbi, kiukweli anafurahia na hali ya kuletewa mbadala jambo ambalo anasema ni vyema kupanua kikosi.

“Tshishimbi ni kati ya wachezaji wenye uwezo mkubwa sana kuichezea Yanga, hivyo hawezi kufikiria kupoteza nafasi yake kama tu afya ipo sawa kama watu wengine wanavyomdhania, kikubwa niwaambie tu kuwa, yeye yupo tayari kuusaidia hata uongozi katika usajili wa kiungo huyo,” kilisema chanzo chetu.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa hesabu za Yanga kwa sasa kwanza ni kuwekeza nguvu nyingi kwenye dua ili Mungu asaidie janga la Corona lipishe kisha ripoti itajadaliwa wakati ukifika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic