April 14, 2020


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umefikia hatua nzuri ya kuipata saini ya nyota wa Simba, Clatous Chama ili akacheze ndani ya Yanga msimu ujao.

Chama amekuwa gumzo kutokana na uwezo wake ndani ya uwanja jambo ambalo limewavutia Yanga ambao wanahitaji kuboresha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa wamezungumza na meneja wa Chama ambaye amesema kuwa mkataba wa nyota huo umebakisha miezi sita.

"Tupo kwenye mpango wa kumpata mchezaji wa Simba na tumezungumza na Meneja ambaye amesema kuwa mteja wake ana miezi sita hivyo ikiwa tunahitaji kumpata ni suala la muda tu," amesema.

Chanzo: Wasafi

3 COMMENTS:

  1. Chama kashahojiwa kasema ni UZUSHI wa mitandao tu.Ana mkataba na Simba.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Watu hawaongei na Mbwa bali na Mwenye Mbwa,hivyo yanga kamwe haitaongea na Chama bali Meneja wake,zuzu mkubwa wewe

      Delete
    2. KWANI BROTHER HUWEZI KUJIBU MPAKA UMDHIHAKI MTU?UNAJUA MAANA YA ZUZU?KWA TAFSIRI YA HARAKA HAPA UNAONEKANA WEWE NDIO ZUZU KWASABABU HUJUI KANUNI ZA USAJILI KAA UKIJUA WAKALA SIO REFA KWAMBA AKIFUNIKA PENATI LAZIMA IPIGWE HAPANA,WAKALA NI MPIGA DEBE TU NA WALA HAWEZI KUINGILIA MASLAHI YA MCHEZAJI,CHAMA ANA MAAMUZI YAKE YEYE KAMA MCHEZAJI SUALA LA WAKALA SIO ISHU KWASABABU HAWEZI KUKULAZIMISHA KUFANYA JAMBO USILOLITAKA,LABDA TU TAFUTA HOJA ZA MSINGI KUTETEA MAELEZO YAKO LAKINI SIO ETI TUNAONGEA NA MWENYE MBWA HA HA HA HA HA HA,THE TIME WILL TELL.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic