May 26, 2020


MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere amerejea leo Dar es Salaam na kupokelwa na Mratibu wa Simba Abass Ally akitokea Rwanda.

Kagere alisepa nchini baada ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa na Serikali Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona.

Amerejea nchini baada ya Serikali kuruhusu ligi kuendelea baada ya kujiridhisha kuwa hali ya maambukizi imeanza kupungua ataungana na wenzake kesho kuanza mazoezi rasmi kwa ajili ya kujiweka sawa kumaliza ngwe ya mechi za ligi kuu itakayoanza Juni, Mosi.

Ametua Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akitoka jijini Mwanza ambapo ndipo safari yake ya kukwea pipa ilianza.

Kagere ni kinara wa kutupia ambapo amefunga mabao 19 na kutengeneza pasi tano za mabao huku Simba ikiwa imefunga mabao 63.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic