May 26, 2020


UONGOZI wa Yanga umewaomba mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo kuungana katika kuitimiza ndoto ya timu hiyo kuelekea kwenye mabadiliko.

Mshindo Msolla, Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga amesema kuwa anaamini katika malengo ambayo ameyaweka yatatimia kwa timu hiyo kuwa katika mfumo wa mabadiliko ya utendaji.

"Ninaamini katika kusimamia yale malengo ambayo nipo nayo hasa katika uongozi na kwa sasa ndoto kubwa ni kuona kwamba klabu inakuwa katika mfumo wa mabadiliko.

"Kwa kushirikiana na wadhamini pamoja na wadau nina amini hili linawezekana hivyo kikubwa ni kushirikiana katika kuelekea kwenye safari ya mabadiliko," amesema.

2 COMMENTS:

  1. Hakuna lolote mabadiliko yepi? Hamna lolote GONGOWAZI

    ReplyDelete
  2. Kama huna cha kuandika si Bora uache? Kwahiyo unataka waje wakuombe wewe ushauri?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic