May 27, 2020


BEKI wa kimataifa wa Tanzania anayecheza katika kikosi cha Highlands Park kinachoshiriki Ligi Kuu Afrika kusini, Abdi Banda, amesema kuwa ana shauku kubwa ya kurejea Tanzania lakini kufungwa kwa mipaka kunakofanyika ili kuchukua tahadhari ya maambukizi ya Virusi vya Corona ndio kikwazo.

Banda amesema kwa sasa wanaendelea na mazoezi huku wakisubiri taarifa rasmi ya Serikali kuhusu Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

“Ni kweli natamani kurudi nyumbani hasa kipindi hiki ligi ikiwa imesimama kwa muda mrefu lakini siwezi kufanya hivyo kwa sasa kutokana na mipaka kufungwa.

“Kuhusu michezo bado tunaendelea na programu zetu za mazoezi ya mmojammoja kama kawaida kuendana na makocha wanavyotutumia huku tukisubiri hiyo taarifa rasmi ya Serikali,” alisema Banda.

Highlands Park iko katika nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu Afrika Kusini baada ya kujikusanyia pointi 31 katika michezo 24 waliyocheza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic