May 13, 2020


HANII Kessy, Meneja wa kiungo wa Simba, Ibrahim Ajibu amesema kuwa nyota huyo sio wa kucheza Yanga ama Azam ana ofa nje ya nchi hivyo wakati ukifika atasepa.

Ajibu amekuwa habati nafasi ndani ya Simba msimu huu tangu alipojiunga na Klabu hiyo akitokea Yanga kut
okana na ushindani mkubwa wa namba.

Kessy amesema:" Ajibu ni mchezaji mzuri, malengo yetu ni kuona kwamba anakipiga nje ya nchi na huko akiwa nje ya Tanzania atapata nafasi ya kucheza.

"Tayari tumeshapokea ofa nyingi za klabu tofauti kutoka nje ila kwa kuwa mteja wetu ana mkataba na Simba tumewaomba wafuate utaratibu wa kuongea na klabu kwanza.

Ajibu msimu huu Simba ikiwa imefunga mabao 63 amehusika kwenye mabao matano, akitoa pasi nne na kufunga bao moja mbele ya Polisi Tanzania Uwanja wa Taifa.

3 COMMENTS:

  1. Yanga na Azam zinamjua mteja wako,mvivu hawamtaki hata bure

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ajibu atafute wakala mwingine huyu anamuinguza kwenye shimo

      Delete
  2. Uyo wakala hamna kitu apo anaua kiwngo kwajili ya mapenzi ya timu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic