KOCHA Mkuu
wa Yanga, Mbelgiji, Luc Eymael, ameweka wazi kufurahishwa na kauli iliyotolewa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, juu ya kufikiria kuruhusu
ligi kuendelea kama kawaida, huku akimtumia ujumbe maalum.
Ligi Kuu
Bara na ligi zingine hapa nchini zimesimama tangu Machi 17, mwaka huu kupisha maambukizi ya
Virusi vya Corona.
Eymael
ambaye kwa sasa yupo Ublegiji kwa mapumziko, amemuomba Rais Magufuli afungue viwanja vya ndege kwa sababu wachezaji na
makocha wa kigeni waliorejea kwao, waweze kurudi Tanzania kuendelea na majukumu
yao.
“Nimesikia Rais
wa Tanzania akisema anafikiria kuruhusu ligi iendelee, unajua Ujerumani na
Italia wanatarajia kuendelea kucheza kuanzia mwezi huu.
“Kwa upande
mwingine, naomba rais afungue viwanja vya ndege kwa ajili ya kupokea ndege za
kigeni, huku Ubelgiji viwanja vya ndege vinatarajia kufunguliwa wiki ijayo,
hata Tanzania inabidi iwe hivyo kwa kuwa baadhi ya wachezaji na makocha wa timu
kama Yanga na Azam wanatakiwa warudi kwa ajili ya kumalizia mechi zilizobaki.
“Kikubwa tutakachofanya
ni kila timu ihakikishe inawaweka wachezaji hotelini na ikitokea wanasafiri
basi wasafiri wakiwa wamejikinga vizuri, uwanjani inabidi uwekwe utaratibu wa
kupima wachezaji, makocha, waamuzi na watu wanaotunza viwanja,” alisema Eymael.
SOURCE: SPOTI XTRA
0 COMMENTS:
Post a Comment