IMEELEZWA kuwa nahodha wa Klabu ya Barcelona Lionel Messi aligomea dili la kujiunga na Klabu ya Inter Milan mwaka 2008.
Kwa mujibu wa kiongozi wa ufundi wa zamani ndani ya Inter Milan, Marco Branca amesema kuwa ilibaki kidogo nyota huyo aibukie ndani ya kikosi hicho.
Branca ameweka wazi kuwa dili hilo lilikuwa kubwa ila lilishindikana kutokana na Messi mwenyewe kugoma kuondoka ndani ya Nou Camp licha ya dili nono mezani.
Kwa sasa kandarasi ya Messi inatarajiwa kumeguka msimu ujao na anatajwa kuwa anaweza kusepa ndani ya klabu hiyo na kuibukia ndani ya Serie A ili kubadili upepo baada ya kudumu muda mrefu ndani ya La Liga.
Messi ameshinda mataji 34 ndani ya Barcelona ikiwa ni 10 ya La Liga na manne ya Ligi ya Mabingwa ulaya. Pia ana Ballons d'Or sita akiwa amefunga jumla ya mabao 627 kwenye mechi 718.
0 COMMENTS:
Post a Comment