May 28, 2020


MAJEMBE ya kazi mengine ndani ya kikosi cha Simba yanatarajiwa kuripoti kambini leo baada ya wengine kuanza kuripoti jana.

Patrick Rweyemamu, Meneja wa Simba amesema kuwa wachezaji watakaoripoti kambini wote watapimwa afya na kuendelea na program nyingine ambazo zitapangwa.

Baadhi ya nyota wa Simba ambao wamesharipoti kambini hawa hapa:-Aish Manula, Beno Kakolanya, Ally Salim, Jonas Mkude, Pascal Wawa, Gadiel Michael, Shomari Kapombe, Meddie Kagere, Mohamed Hussein, Miraj Athuman.

 Said Ndemla, Deo Kanda, Hassan Dilunga, Rashid Juma,Haruna Shamte,Yusuph Mlipili, Kenedy Juma,Tairone Santos, Gerson Fraga, John Bocco, Luis Misqussone, Shiza Kichuya na Erasto Nyoni.

1 COMMENTS:

  1. Hao waliokwishafika ni kikosi kinachotosha kabisa cha kumpinduwa chali kila ataejaribu kubaki njiani na kujaribu kutokipisha njia. Au vipi Al Hashmi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic