
MAJEMBE maane haya ya kimataifa yamekubali kutua ndani ya Yanga iwa[o utaratibu utafuatwa.
Taarifa zimekuwa zikieleza kuwa Yanga ipo kwenye rada za kuwanasa nyota kadhaa ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho cha mabingwa watetezi.
Hivyo kwa lugha ya kitaa wanasema Yanga washindwe wenyewe kwani majembe hayo yamekubali kutua nayo ni haya hapa:- Sven Yidah yeye ni
kiungo anakipiga ndani ya Kariobang Sharks.
Tuisila Kisinda yeye ni winga anakipiga ndani ya AS Vita.
Michael Sarpong yeye ni mshambuliaji raia wa Ghana anayekipiga ndani ya Rayon Sports ya Rwanda yeye ni mshambuliaji.
Mussa Mohamed yeye ni beki anakipiga ndani ya Nkana FC.
Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Hersi Said aliweka wazi mpango wa kampuni hiyo inayoidhamini Yanga kufanya usajili wa maana ndani ya timu hiyo. "Muda wa usajili ukifika kila kitu kitakuwa wazi,".







UTOPOLO KILA MCHEZAJI WA KWENU MNATISHA.
ReplyDelete