UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mchakato wa safari ya kuelekea mabadiliko umefika hatua nzuri na mpango mkubwa uliopo ni Mei 31 itakuwa siku maalumu ya kutiliana saini kati ya Yanga, GSM na La Liga ya Hispania.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Uhamasishaji na Msemaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kukamilisha hatua za mwisho kabla ya shughuli yenyewe.
"KIla kitu kipo sawa kwa sasa tunasubiri wakati ufike tu kwani mambo ya La Liga na GSM sio ya mchezo, kikubwa ni kuwaomba tu mashabiki wasikose kutazama Azam TV ama kufuatilia kupitia Yanga TV tutakuwa mubashara.
"Hatua kwa hatua tunakwenda taratibu bila papara tunajua kile ambacho tunakitafuta," amesema.
Dai
ReplyDeletema mbele nyuma mwiko