UONGOZI wa
Yanga umesema kuwa hesabu kubwa ni kuona ndoto za safari ya mabadiliko inatimia
kwa kuwa ni mpango mkubwa uliopo kwenye majalada ya Yanga.
Yanga
imeanza mchakato wa kuelekea kwenye mabadiliko ambapo mchakato huo ulisimama
kwa muda kutokana na janga la Virusi vya Corona ambavyo vinaivuruga dunia.
Mshindo
Msolla, Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga amesema kuwa ni wakati wa mashabiki na
wadau kuunga mkono mpango wa mabadiliko ili kufikia ndoto waliyokuwa wakiiota
muda mrefu.
“Imani kubwa
ni kuona kile ambacho tunakiota kwa muda mrefu kitatimia kwani tunashirikiana
na wadhamini wetu hatua kwa hatua pamoja na wadau mbalimbali, lengo letu ni
kuona kwamba tunakuwa kwenye mfumo mpya ambao utakuwa na matokeo chanya kwetu
kikubwa ni sapoti,” amesema Msolla.








0 COMMENTS:
Post a Comment