May 16, 2020

PAUL Nonga, nahodha wa Klabu ya Lipuli inaelezwa kuwa yupo kwenye rada za mabosi wake wa zamani Yanga ambao wanataka kurejesha saini yake.

Nonga aliwahi kukipiga ndani ya Yanga enzi za Hans Pluijm aliomba kusepa ndani ya kikosi hicho baada ya kukosa namba kikosi cha kwanza ila kwa sasa amekuwa bora ndani ya Lipuli.

Msimu huu Nonga amevunja rekodi yake ya mabao ya msimu uliopita 2018/19 ambapo alifunga mabao matano huku msimu huu wa 2019/20 akitupia mabao 11 jambo linalowapa matumaini Yanga kuiwinda saini yake. 

 Nonga amesema kuwa ana dili nyingi mkononi ila hawezi kutaja kwa sasa atasaini wapi kwani tayari ameshawaaga mabosi zake Lipuli. "Nimeshawaaga mabosi zangu Lipuli ili watafute mbadala mwingine ila nitakapoibukia nitajua mwenyewe wakati ukifika," amesema Nonga.

2 COMMENTS:

  1. Viongozi wa Yanga wakimsajiri Nonga watakua mazumbukuku na wasio jua walitendalo,Nonga si mchezaji wa kucheza Yanga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakubaliana nawe ndugu... Kule lipuli anaonekana kufanya vizuri kwasababu anacheza bila presha ya mashabiki. Huku Yanga alishindwa kucheza sababu hiyo ya mashabiki. Wasimchukue atakuja kukaa benchi tuu

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic