GERALD
Mdamu, mshambuliaji namba moja ndani ya Mwadui FC anayeshikilia rekodi ya kuwatungua makipa wote
wa Simba, Aishi Manula na Beno Kakolanya amekimbia zake makao makuu ya nchi,
Dodoma na kuibukia Songea vijijini kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.
Mdamu
alianza kumtungua Aishi Manula kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara wakati Simba ikipoteza
kwa kufungwa bao 1-0 kisha akamalizana na Beno Kakolanya kwenye mchezo wa Kombe
la Shirikisho wakati Mwadui ikifungwa mabao 2-1.
Mdamu amesema kuwa hali haijawa shwari kwa sasa kutokana
na hofu iliyotanda dhidi ya kusambaa kwa Corona jambo lililomfanya asepe makao
makuu ya nchi.
“Bado mambo
hayajawa sawa kwa sasa ni tahadhari na mazoezi, nilikuwa Dodoma ila nimeondoka mpaka huku Songea vijijini ninaendelea kuchukua tahadhari na kufanya
mazoezi, nimefurahi kuskia ligi inatarajiwa kurudi hivyo lazima nijiweke sawa,”
amesema Mdamu.
Mwadui FC
ikiwa nafasi ya 12 na pointi zake 34 kwenye mabao 27 amehusika katika mabao
nane ambapo amefunga matano na kutoa pasi tatu za mabao.
Chanzo ni Championi







0 COMMENTS:
Post a Comment