SARAKASI za usajili huwa zinakuwa zina mambo mengi hasa kwa wachezaji kusaini kwenye timu mbili kutokana na ushawishi wao ama kushindwa kuwa na wasimamizi wazuri.
Miongoni mwao ambao waliwahi kupatia wapo nyota ambao bado wanawika na wengine wapo nje ya nchi kukipiga baadhi yao ni hawa hapa:-
Pius Buswita
Alikuwa na mikataba miwili wa Yanga na Simba. Inaelezwa kuwa alianza kusaini mkataba wa Simba kisha baaaye akamalizana na Yanga msimu wa 2017/18.
Jambo lililosababisha apelekwe kwenye kamati ya Katiba Sheria na hadhi za Wachezaji TFF iliyokutana Agosti 20 na 21 ,2017.
Baada ya mvutano Klabu za Simba na Yanga zikakubaliana kulinda Kipaji Cha kijana Buswita Yanga walikubali kuilipa Ile fedha ya usajili ambayo Simba waliitoa Kisha Buswita akarejea Uwanjani kuitumikia Yanga.
Hassan Kessy
Ni moja Kati ya mabeki bora wa kulia Tanzania ambaye anakipiga Zambia. Listi hii haijamuacha salama Kessy kwani naye aliingia matatani mwaka 2016 baada ya kusaini mkataba na Yanga huku bado akiwa na mkataba na Simba.
Ushahidi wao Simba ulikuwa ni picha zilizokuwa zikimuonesha Kessy akisaini Yanga. Lakini pia zingine picha zilimuonesha akiwa Uwanja Wa Ndege kwenye msafara na wachezaji wengine Wa Yanga waliokuwa wakienda nje ya nchi. Kutokana na uvunjifu huo wakanuni Yanga walilazimika kuilipa Simba Sh Milioni 50 ili Kessy abaki Yanga.
Venance Ludovic
2017 alikutana na balaa la kukosa mechi nne za Klabu ya African Lyon baada ya kufungiwa kwa kosa la kusaini ndani ya klabu hiyo ilihali bado alikuwa na mkataba na Mbao FC.
Adhabu yake mwishoni ilibatilishwa baada ya kugundulika kuwa ameonewa.
Mohamed Mkopi
Nyota wa zamani wa Tanzania Prisons,2016 alikuwa na madili sehemu mbili. Alisaini ndani ya Mbeya City ilihali ana mkataba na Prisons. Alifungiwa mwaka mzima kutojihusisha na mpira.
Feisal Salum
Ufundi wa Fei Toto ulionekana akiwa na jezi ya Zanzibar Heroes katika michuano ya kombe la Afrika Mashariki na Kati yaani challenge Cup mwaka 2018. Baada ya hapo klabu mbalimbali zikaonesha nia ya kutaka huduma yake. Singida ilifanikiwa kuwa ya kwanza kabla ya Yanga kumdakia juujuu hali iliyoleta mtafaruku.
Baadaye ulimalizwa na maongezi, na maongezi hayo yalifanikiwa kwa msaada mkubwa wa Mwenyekiti wa Singida United ambaye pia ni shabiki mkubwa wa Yanga Dk.Mwigulu Nchemba na hivyo Fei Toto kuruhusiwa kukipiga Jangwani.
Mrisho Ngassa
2013 akiwa mchezaji wa Azam FC kwa mkopo akitokea Simba alisaini dili kwa siri ndani ya Yanga.
Alifiksihwa kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) alitakiwa kulipwa milioni 45 ili aweze kucheza ndani ya Yanga ndicho alichokifanya.
0 COMMENTS:
Post a Comment