May 17, 2020

WACHEZAJI hawa watano wamekubali jumlajumla kutua ndani ya Klabu ya Simba kukipiga msimu ujao iwapo utaratibu utafuatwa:- Jemmy Mumbere yeye ni kiungo wa AS Vita amesema kuwa Simba ni timu kubwa iwapo masuala yatakwenda sawa hana hiyana atamwaga wino na kazi atapiga.

Justin Shonga, yeye ni winga anakipiga ndani ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini amesema kuwa ikiwa ni kweli Simba wanahitaji saini yake basi waongee na uongozi wa timu kisha kazi itapigwa. 
Jackson Lunaga ni mlinda mlango wa AS Vita na timu ya Taifa ya Congo yeye amesema anatamani kucheza na Deo Kanda mshikaji mwenzake anayekipiga Simba.

Bakari Mwamnyeto miongoni mwa wazawa chipukizi wanaofanya vema ndani ya Uwanja akikipiga Coastal Union amesema timu itakayofuata utaratibu hana tatizo nayo.

Baraka Majogoro,  kiungo wa Polisi Tanzania amesema sitafikiria kukataa ofa ya Simba kwa kuwa ni timu kubwa.

4 COMMENTS:

  1. Si mlisema Manyeto 100% Yana mbona sasa mwageuza maneno?

    ReplyDelete
  2. Enter your comment...MNAONYESHA HAMKO ACTIVE KTK KAZ! MLISEMA MWAMNYETO 100% NI YANGA NA MAMBO YAMEISHA LEO MNAMTAJA TENA SIMBA JAMAN HIZI BLOG ZTAISHIA KUWAPA WATU UGONJWA WA PRESHA TU!

    ReplyDelete
  3. Msipende kuipakazia Simba kuhusu usajili. Simba bado haijaanza mipango hiyo, labda Utopolo huko.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic