May 27, 2020




MWENYEKITI wa zamani wa Klabu ya Simba, Ismael Aden Rage ambaye juzi alishikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za rushwa na kuanza kampeni za uchaguzi mkuu kabla ya wakati kabla ya kupewa dhamana amesema kuwa hakukutwa akitoa hela .

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Tabora, Mussa Chaulo ilisema kuwa mnamo Mei 23, 2020, Rage ambaye ni Mkurugenzi wa Voice of Tabora alishikiliwa baada ya TAKUKURU kupata taarifa kutoka chanzo cha siri kikieleza kuwa Mbunge huyo wa zamani wa Tabora Mjini amedaiwa kuanza kampeni za uchaguzi kabla ya wakati.

Ili kutoharibu uchunguzi unaondelea, Rage aliwekwa mahabusu kuanzia Mei 23 hadi Mei 24 ambapo aliachiwa kwa dhamana.

“Uchunguzi wa taarifa hii unaendelea na mara utakapokamilika taarifa kamili itatolewa kupitia vyombo vya habari,” ilieleza taarifa hiyo ya Mkuu wa Takukuru mkoa Tabora, Mussa Chaulo.

Rage alisema kuwa : “Mimi TAKUKURU hawajanikuta mahala popote natoa hela wala hawajanikuta popote na wanachama wa CCM. Walinifuata nikiwa nafuturu wakaniambia alhaji wewe malizia futari halafu tutazungumza,” alisema Rage.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic