UONGOZI wa
Singida United umesema kuwa umebakiza dakika 810 za moto zitakazotoa hatma yao
ya kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kutokana na mwendo wao kuwa wa kusuasua.
Akizungumza
na Championi Jumamosi, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana alisema
kuwa kurejea kwa ligi ni ishara ya wao kurejea vitani kumaliza kazi yao
waliyoianza.
“Tuna mechi
tisa mkononi ambazo zimebaki hizo zote ni mwendo wa kufa na kupona kwani tuna
kazi kubwa ya kufanya ili kubaki ndani
ya ligi ukizingatia kwamba ushindani ni mkubwa.
“Mpango
mkubwa ni kuona kwamba kila mechi tunacheza mithili ya fainali itakuwa njia
pekee ya kutufanya tubaki msimu ujao kwa sasa tunaanza maandalizi ili kurejea
vizuri,” alisema Katemana.
Singida
United ipo nafasi ya 20 ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi 29 ikiwa
imepokea vichapo mechi 20.







0 COMMENTS:
Post a Comment