SVEN
Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amechanganywa na dakika 508 za kiungo wa Simba, Miraj Athuman
‘Sheva’ kutokana na data zake kuonyesha kuwa ametumia muda mchache kufanya
mambo makubwa uwanjani.
Sheva
amefunga mabao sita na kutoa pasi moja ya bao huku akisababisha penalti mbili
ndani ya ligi ambapo zote zilifungwa na Meddie Kagere ilikuwa mbele ya Kagera
Sugar na Mbeya City.
Sven
amesema:”Miongoni mwa wachezaji ambao wanaonekana kuwa bora ni Miraj lakini
sijamtumia kutokana na majeraha yake, nina imani akirejea kwenye ubora wake
atakuwa na vingi vya kufanya.”
Sheva kwa
sasa anatibu jeraha lake la funda la goti ambalo aliumia mwaka jana akiwa na
timu ya Taifa ya Tanzania hali yake imeanza kutengamaa.
Mechi
alizocheza ni tisa kati ya 28 ambazo ilikuwa namna hii:-JKT Tanzania (30), Mtibwa
Sugar (27) Kagera Sugar, (29), Biashara United (83), Azam FC (33), Singida
United, (81), Mwadui (45), Mbeya City (90), Ruvu Shooting (90).







0 COMMENTS:
Post a Comment