May 25, 2020


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Tabora imesema ilimkamata na kumuhoji Mkurugenzi wa Voice of Tabora, Ismael Rage ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba kwa tuhuma za kuanza kampeni za Uchaguzi Mkuu kaba ya wakati.

 Rage anadaiwa kukusanya viongozi wa CCM wa kata na matawi kwa lengo la kuwashawishi wampigie kura baada ya TAKUKURU kupata taarifa kutoka chanzo cha siri kikieleza kuwa mbunge huyo wa zamani wa Tabora Mjini ameanza kampeni za uchaguzi kabla ya wakati.

Taarifa ya Takukuru inasema Rage ambaye ameachiwa kwa dhamana na uchunguzi wa suala lake utakapokamilika taarifa kamili itatolewa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic