May 12, 2020


INAELEZWA kuwa thamani ya beki wa Coastal Union,  Bakari Mwamnyeto inafika milioni 85 hivyo timu inayomtaka ivunje benki kuweka mkwanja huo mezani.

Beki huyo chipukizi anavaa kitambaa cha unahodha ndani ya klabu hiyo iliyo chini ya Kocha Mkuu, Juma Mgunda.

Miongoni mwa timu ambazo zinatajwa kuiwinda saini yake ni pamoja na Simba iliyo chini ya Sven Vandenbroec pamoja na Yanga iliyo chini ya Luc Eymael wote ni raia wa Ubelgiji.

Pia matajiri wa Bongo, Azam FC wanatajwa kuwa kwenye hesabu za kuwania saini yake ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho ambao ni Mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho.

Mwamnyeto amesema:"Nimekuwa nikiskia taarifa hizo ila hakuna kitu kinachoendelea nipo zangu bado ndani ya Coastal Union,".

2 COMMENTS:

  1. Porojo porojo za kila siku,hamchoki?

    ReplyDelete
  2. Mwenye benki kubwa na pia mapenzi kuliko wote apishwe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic