JANGA la Virusi vya Corona limeacha balaa kubwa katika klabu
mbalimbali barani Ulaya ikiwemo Barcelona ambapo imepanga kuuza mastaa wake akiwemo Luis
Suarez ili kujiingizia fedha.
Kutokana
na La Liga kusimama hivi sasa huku ikitarajiwa kurudi kwa kuchezwa bila ya
mashabiki, Barcelona inaangalia njia mbadala ya kupata vyanzo vya mapato ndiyo
maana inataka kuuza mastaa wake.
Klabu
mbalimbali zinazoshiriki
Ligi Kuu ya Marekani (MLS), zinatajwa kumuwania kwa nguvu Suarez.
Mmiliki
wa Klabu ya Inter Miami, David Beckham,
amenukuliwa akisema kuwa, atafurahi kuona nyota huyo akitua kwao.
Hivi
karibuni, Suarez alisema: "Huwezi jua, bado nina mkataba na Barcelona, lakini kwa mustakabali wa maisha ya baadaye,
naona Ligi ya Marekani inavutia sana kwangu, ni sehemu nzuri."
Mkataba
wa Suarez ndani ya Barcelona unaenda hadi 2021 ambapo kuna
kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi chenye masharti ya kucheza mechi kwa
asilimia 60 msimu ujao.
0 COMMENTS:
Post a Comment