WACHEZAJI
wa Real Madrid, wanatarajiwa kuanza mazoezi Mei 11, mwaka huu ambapo yatakuwa mazoezi binfasi.
Mazoezi
hayo yatafanyika kwa uangalizi maalum huku yakiwa na wachezaji na makocha wachache.
Wachezaji
mbalimbali wa La Liga, wiki ijayo wanatarajiwa kupimwa afya zao kuonekana kama
hawana maambukizi ya corona.
Hatua
hiyo imekuja ikiwa ni kuona kila mmoja anakuwa salama kuanzia wachezaji hadi
makocha kabla ya kuanza mazoezi ya pamoja na kucheza michezo ya La Liga.
Kwa
sasa wachezaji wote wa Real Madrid, wataendelea kufanya
mazoezi binafsi hadi hapo Mei 11, ambapo watatakiwa kwenda kwenye viwanja vyao
vya mazoezi vijulikanavyo kama Valdebebas.
0 COMMENTS:
Post a Comment